Na Mwandishi Wetu - Dodoma
Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa program ya maadhimisho ya miaka 100 ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dodoma Waziri wa Maliasili na Utakii Dkt Damas Ndumbaro amesema    maathimisho hayo ya kumuenzi  Hayati Mwalimu Nyerere  ni sehemu ya mpango wa miaka 10 kwa kuenzi na kusherehekea urithi wa maisha ya Muasisi huyo wa Taifa.

DKT Ndumbaro amesema maathimisho hayo yatashirikisha wadau ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu mchango wa Mwalimu Nyerere Kitaifa na Kimataifa na umuhimu wa kuandaa, kutangaza na kumuenzi, kukusanya, kuendelez, kuhifadhi na kutangaza rasilimali za urithi wa Mwalimu Nyerere kwa manufaa ya Kizazi Cha Sasa na kijacho ili kukuza na kuendeleza utalii.

Maathimisho hayo yanatarajiwa kufikia kilele tarehe 13 April 2022 Butiama Mkoani Mara, ambapo tarehe hiyo ni siku ya  kukumbuka kuzaliwa kwa muasisi huyo na endapo angekuwa hai angetimiza miaka 100.

Waziri Ndumbaro amesema kuelekea kilele hicho matukio mbalimbali yanatarajiwa kufanyikaikiwa ni pamoja na mikutano ya wadau, mashindano ya baiskeli, matembezi ya hiari, ngoma za asili na Mwalimu Nyerere marathoni itakayofanyika kabla ya tarehe hiyo ya 13 April 2022.
Maathimisho hayo yataendelea kufanyika kila mwaka ifikapo tarehe hiyo.

Hata hivyo Waziri Ndumbaro amesema Wizara itawatangazia wananchi utaratibu  utakaofuatwa ili wale wenye uwezo wa kutengeneza nembi wawalilishe maombi kwa ajili ya kushiriki kwenye shindano la kutengeneza nembo ya Mwalimu Nyerere.