Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekataa ofa ya Marekani ya kumsaidia kuondoka Ukraine, vyombo vya habari vya Marekani vinasema.
"Mapambano yamefika. Nahitaji risasi, sio msaada wa kuondoka", shirika la habari la Associated Press limesema, likimnukuu afisa mkuu wa kijasusi mwenye ufahamu wa moja kwa moja wa mazungumzo hayo.
Gazeti la Washington Post pia lilikuwa limewataja maafisa wa Marekani na Ukraine ambao walisema kuwa serikali ya Marekani iko tayari kumsaidia Bw Zelensky.