Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametengua uteuzi wa Kamishna Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Salum Yussuf Ali, ili kupisha uchunguzi wa kina wa upotevu wa fedha za makusanyo ya mapato zilizopotea.

Rais Dkt. Mwinyi amefikia maamuzi hayo leo wakati akiwa katika Ofisi za Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Mazizini Zanzibar ambapo alipata fursa ya kuzungumza na uongozi wa Bodi ya Mapato, Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mapato pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA), mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mamlaka hiyo.

Wakati huo huo, taarifa maalum iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said ilieleza utenguzi wa kiongozi huyo alioufanya Rais Dkt. Mwinyi  Februari 17, 2022.