Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza "operesheni ya kijeshi" katika eneo la Donbas nchini Ukraine.

Alitoa tamko hilo katika hotuba ya televisheni huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likimsihi aache.

Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni , Putin anawataka wanajeshi wa Ukraine katika eneo la mapigano mashariki mwa Ukraine kuweka silaha chini na kurejea majumbani mwao.

Aliionya Ukraine kwamba italaumiwa kwa umwagikaji wa damu wowote.

Putin pia anasema "haki na ukweli" ziko upande wa Urusi, akionya kwamba jibu la Moscow litakuwa "papo hapo" ikiwa mtu yeyote atajaribu kuchukua dhidi ya Urusi.

Rais wa Urusi pia anasema hatua za nchi yake ni kujilinda na kuwaambia wanajeshi wa Ukraine baba zao na babu zao hawakupigana ili waweze kuwasaidia Wanazi mamboleo.