Rais wa Urusi Vladimir Putin ameamuru jeshi la Urusi kuweka vikosi vyake vya nyuklia katika "tahadhari maalum" - kiwango cha juu cha tahadhari kwa Vikosi vya Kimkakati vya Kombora vya Urusi.

Akizungumza na maafisa wakuu wa kijeshi, akiwemo Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu, amesema mataifa ya Magharibi yamechukua "hatua zisizo za kirafiki" kwa Urusi na kuweka "vikwazo visivyo halali".

Rais wa Urusi Vladmir Putin ameamuru usimamizi wa jeshi kuweka kikosi maalum cha nyuklia katika hali "maalum" ya tahadhari.

Hii ni baada ya kile ambacho Moscow inakiita "taarifa za uchokozi" za nchi za muungano wa Nato.

Kiongozi huyo wa Urusi tayari alikuwa ametoa onyo kwamba yuko tayari kutumia silaha za nyuklia kama nchi za magharibi zitamuingilia katika mgogoro wa Ukraine.

Wiki iliyopita, alionya kwamba "yeyote anayejaribu kutuzuia" ataona matokeo "hujawahi kuona katika historia yako".