Serikali imesema vichwa vya treni ya umeme vilivyoagizwa bado havijawasili nchini. Imesema vichwa hivyo vipo kiwandani vinatengenezwa, kilichoingia nchini ni cha wakandarasi kwa ajili ya kufanyia majaribio.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa baada ya kuibuka mjadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kichwa cha treni kilichoingia nchini.

Katika ukurasa wake wa twitter, Msigwa ameandika: “MSIPOTOSHE. Vichwa vya treni ya umeme vilivyoagizwa na Serikali bado havijawasili nchini, bado vipo kiwandani vinatengenezwa. Kichwa cha treni ya umeme kilichokuja ni cha wakandarasi kwa ajili ya majaribio ya reli ya kisasa ya SGR.”