Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ametoa muda wa miezi sita kukamilisha Mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara  ambapo awali ujenzi huo ulisimama kwa takribani miaka 20.

Akizungumza baada ya kukagua Mradi huo, IGP Sirro, amesema kuwa Umaliziaji wa jengo hilo unatokana na fedha kiasi cha Bilioni 1.4 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Wakati huo huo akiwa Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya IGP Sirro pia amekagua Mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya kamanda wa Polisi ambapo ndani ya siku 100 tangu kutolewa kwa fedha kiasi cha bilioni 1.5 ujenzi huo umefikia hatua mbalimbali za kukamilika.