Afisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Mahabusu ya Watoto kilichopo Kabwe Kata ya Iyela Jijini Mbeya Groria Kibira(38), amekutwa ameuawa kwa kunyongwa na watu wasiojulikana kwenye nyumba yake iliyopo ndani ya eneo la Kituo cha Mahabusu hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Ulrich Matei, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mpaka sasa watu wawili wanashikiliwa kwa mahojiano ili kubaini chanzo cha mauaji.

"Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Bukoba Kagera kwa ajili ya maziko" amesema Matei.