TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Mjini Nzega (NZUWASA) anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kuja za nafasi nane (08) kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.

1.0   MWAJIRI: MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI NZEGA (NZUWASA)

1.0.1  AFISA UGAVI DARAJA LA II - (NAFASI
1)

1.0.2  MAJUKUMU YAKAZI

i.       Kukusanya  takwimu za kusaidia kutayarisha makisio ya vifaa vinavyohitajika na

Mpango wa Ununuzi;

ii.       Kukusanya na kutunza takwimu za utendaji kazi za Wazabuni mbalimbali;

iii.       Kusimamia ukaguzi wa hesabu za vifaa mara kwa mara;

iv.       Kusimamia upatikanaji wa vifaa kutoka kwa wa zabuni;

v.       Kutathmini vifaa vinavyotumika katika kila Idara;

vi.       Kutayarisha taarifa za kazi katika vipind maalum; na

vii.       Kutunza kumbukumbu za Manunuzi zinazohusu mchakato wa manunuzi.


1.0.3  SIFA ZA MWOMBAJI
Shahada ya kwanza katika Usimamizi wa Ununuzi na Ugavi kutoka kwa taasisi inayotambuliwa na Serikali.

1.0.4  MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D

1.0.5  MTUNZA KUMBUKUMBU MSAIDIZI DARAJA LA II (NAFASI 1)

1.0.6  MAJUKUMU YAKAZI

i.       Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji;

ii.       Kuthibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka;

iii.       Kuchambua na kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika kwa ajili ya matumizi ya ofisi;
iv.       Kupanga nyaraka katika masjala;

v.       Kuweka kumbukumbu katika mafaili; na

vi.       Kushughulikia maombi kutoka Taasisi za serikali.

1.0.7  SIFA ZA MWOMBAJI

Awe na cheti cha Kidato cha IV na Diploma katika usimamizi wa rekodi

1.0.8  MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C

1.0.9    MHANDISI WA MAJI DARAJA LA II (NAFASI 1)

1.0.14 MAJUKUMU YAKAZI

i.     Kufanya kazi kwa vitendo katika fani zinazomhusu ili kumwezesha Mhandisi kupata sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi;
ii.     Kushiriki kutengeneza michoro/ ramani za miradi ya maji; na iii.     Kushiriki katika shughuli za ujenzi wa miradi ya maji.

1.0.15 SIFA ZA MWOMBAJI

Shahada ya kwanza ya Uhandisi wa Mazingira aliyesajiliwa na Bodi ya Usajili ya Wahandisi wa Tanzania. Lazima awe na ujuzi wa matumizi ya Kompyuta na ujuzi wa usimamizi.

1.0.16 MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS E

1.0.17 AFISA TEHAMA DARAJA LA II (NAFASI 1)

1.0.18 MAJUKUMU YAKAZI

i.     Kufanya usanifu wa kila siku, kusasisha, utatuzi na matengenezo ya kompyuta, programu na vifaa vya pembeni (kama vile vichapishi, skana);
ii.      Kufanya usimamizi wa mitandao ya Mamlaka, intraneti na muunganisho wa intaneti;
iii.     Kufanya kazi zote za kiufundi zinazohusu matumizi ya huduma za IT na vifaa kwa watumishi;
iv.     Kusaidia katika uhifadhi wa hifadhi data ya Mamlaka na vifaa vya uhifadhi na mifumo ya pili;
v.     Kuendesha na kutunza katika hali nzuri vifaa na mifumo yote iliyowekwa kwenye Mamlaka; na

vi.     Kupanga ratiba za matengenezo ya kuzuia ya kompyuta na vifaa vinavyohusiana.

1.0.19 SIFA ZA MWOMBAJI

Shahada ya Sayansi ya Kompyuta kutoka kwa Taasisi inayotambuliwa na Serikali.

1.0.20 MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D


1.0.21 AFISA HESABU DARAJA LA II (NAFASI 1)

1.0.22 MAJUKUMU YAKAZI

i.     Kuthibitisha ankara za wasambazaji kwa malipo;

ii.     Kutayarisha   ripoti   za   kila   siku   za   malipo   yaliyofanywa   na   makusanyo yaliyopokelewa;
iii.     Kutunza na kuboresha rejista za wadaiwa;

iv.     Kushiriki katika utayarishaji wa hesabu za mwaka; na

v.     Kushiriki katika utayarishaji wa taarifa za utendaji wa fedha za kila mwezi, robo mwaka na mwaka.

1.0.23 SIFA ZA MWOMBAJI

Shahada ya Kwanza katika fani ya Uhasibu au Biashara ya Fedha kutoka kwa taasisi inayotambuliwa na Serikali.

1.0.24 MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D

1.0.25 MSAIDIZI WA HESABU DARAJA II (NAFASI 1)

1.0.26 MAJUKUMU YAKAZI

i.       Kuandika na kutunza register za uhasibu;

ii.       Kuandika hati za Malipo na hati za  mapokezi ya fedha;

iii.       Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu;

iv.       Kupeleka nyaraka za uhasibu Benki; na

v.       Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za kibenki na Amana.

1.0.27 SIFA ZA MWOMBAJI

Stashahada ya Uhasibu, ATEC Level II kutoka kwa kutambuliwa kutoka Taasisi inayotambuliwa na Serikali.

1.0.28 MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C

1.0.29 DEREVA DARAJA LA II

1.0.30 MAJUKUMU YAKAZI

i.       Kuhakikisha kuwa magari yote na vifaa vingine vinawekwa chini ya ulinzi;

ii.       Kukagua magari kabla na baada ya safari;

iii.       Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali katika safari za kikazi;

iv.       Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;

v.       Kufanya usafi wa gari;

vi.       Kufanya ukarabati na matengenezo madogo madogo ya Magari; na vii.       Kuweka na kusasisha kumbukumbu za Logbook.

1.0.31 SIFA ZA MWOMBAJI

Cheti cha kidato cha IV, Leseni ya Udereva Daraja C ya uendeshaji magari ya aina yote, Cheti cha udereva kutoka NIT au chuo kinachotambulika na Serikali.

1.0.32 MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B

MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i.     Waombaji wote wawe ni Raia waTanzania na wenye umri usiozidi miaka 45. ii.     Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii.     Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv.     Waombaji  waambatishe  maelezo  binafsi  yanayojitosheleza  (Detailed  C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatuwa kuaminika.
v.     Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
-   Postgraduate/ Degree/ Advanced Diploma/ Diploma/ Certificates.

-   Cheti cha mtihani wa kidato cha IV naVI

-   Computer Certificate

-   Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
vi.     Testmonials”,“Provisional Results”,“Statement of results”,hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTSSLIPS)HAVITAKUBALIWA.
vii.     Waombaji   waliosoma   nje   ya   Tanzania   wahakikishe   vyeti   vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
viii.     Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibalichaKatibuMkuuKiongozi.
ix.     Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yaliyo katika Waraka Na.CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.

x.     Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi.     Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 27 Januari, 2022.

Muhimu,  kumbuka  kuambatisha  barua  yako  ya  maombi  ya  kazi  iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA S.L.P. 2320 DODOMA.
i.    Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment

Portal) kupitia anuani ifuatayo;

http://portal.ajira.go.tz/

(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘RecruitmentPortal’)


ii.    Maombi yatakayo wasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili

HAYATAFIKIRIWA.


Limetolewa na;

KAIMU KATIBU

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA