Spika wa Bunge, Job Ndugai amemuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote kwa namna yoyote ambayo alihisiwa kutoa neno la kumvunja moyo Rais .

Spika Ndugai amesema hayo leo Jumatatu, Januari 3, 2022 wakati akizungumza na wanahabari kufuatia taharuki iliyoibuka mitandaioni baada ya video yake kusambaa.

“Kwa hiyo binafsi yangu popote pale ambapo nilihisiwa kwamba nimetoa neno la kumvunja moyo Rais wetu na akavunjika moyo, ninatumia fursa hii kumuomba radhi sana mheshimiwa Rais na Watanzania wote. “amesema Ndugai

Amesema kuwa hotuba yake haikuwa na jambo la kukashifu wala kudharau juhudi za Serikali bali alikuwa anasisitiza ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali.