Soko la wafanyabiashara wadogo la Karume lililopo Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam limeungua kwa moto alfajiri ya leo 
huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijulikani.
 

Kufuatia mkasa huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla amewataka wafanyabiasha wa soko  hilo  kuwa watulivu huku akiahidi kuundwa kamati itakayochunguza kujua chanzo cha moto huo.

Makalla amesema hayo leo Jumapili Januari 16, 2022 alipotembelea eneo hilo na kukagua athari za moto huo.

Imeelezwa kuwa moto huo ulioteketeza sehemu kubwa ya soko hilo lenye wafanyabiashara zaidi ya 3,500 ulianza usiku wa kuamkia leo huku Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likijitahidi kuuzima lakini uliteketeza soko hilo sehemu kubwa.

Akiwa akiwa kwenye eneo hilo Makalla amesema "Nawapa pole wafanyabishara wote kwa ajali hii ya moto, hatujajua chanzo kwa kuwa yanaelezwa mengi. Nawaomba kuweni watulivu katika kipindi hiki ambacho tunaunda kamati itakayochunguza kujua chanzo," amesema