Shirika la Afya Duniani, WHO limesema linachunguza kidonge cha molnupiravir Merck cha kutibu ugonjwa wa COVID-19 na litatoa mapendekezo mwanzoni mwa mwezi ujao wa Februari.
Janet Diaz anayesimamia idara ya huduma za afya ndani ya WHO, amesema kuwa idara inayosimamia miongozi ya shirika hilo pia inajiandaa kukitathmini kidonge hicho cha kampuni ya kutengeneza dawa ya Pfizer.
Jana jioni jopo la WHO lilipendekeza matumizi ya dawa mbili zinazotengenezwa na kampuni ya dawa ya Eli Lilly, GlaxoSmithKline na Vir Biotechnology kwa ajili ya wagonjwa wa COVID-19.
Akizungumzia kuhusu matibabu ya seli za kinga ya mwili, Diaz amesema baadhi ya seli zinaonyesha kutokuwa imara katika kupambana dhidi ya aina mpya ya virusi vya corona ya Omicron ambazo hazionyeshi ufanisi mzuri.