Hakika maneno mazuri husadifu mambo mengi mazuri baina yenu ikiwemo upendo, kujali, kuthamini, heshima, utii, upole, nidhamu, uaminifu, unyenyekevu, usikivu, ukarimu na faraja hivyo ni vema kuhakikisha kama kweli unampenda kinywa chako daima kimtolee lugha nzuri ya maneno matamu.

1. Nakupenda
Nakupenda ni kitu rahisi na cha wazi cha kumwambia mwenza wako. Hakikisha tu kuwa unamaanisha. Jaribu kulisema neno hilo pindi mwenza wako anapokuchekesha au pale anapofanya kitu kinachokukumbusha kwanini mko pamoja.....```

2. Umependeza
Kama umekuwa kwenye ndoa kwa muda mrefu, ni rahisi kujisahau katika mengi. Ni muhimu kumkumbusha mwenza wako kuwa anakuvutia. Kumjulisha kuwa ulivo vaa umependeza sana’ kutamfanya ajisikie vizuri na kukumbusha kwanini ulimchagua yeye.

3. Samahani
Kila mtu hukosea wakati fulani. Wakati mwingine hujikuta tukiongea maneno kwa hasira na baadaye kugundua kuwa hatukuwa sahihi. Ubishi hauna nafasi kwenye ndoa ya wenye furaha, hivyo omba msamaha unapofanya kosa. Omba msamaha kwa kukasirika. Omba msamaha kwa kuumiza hisia za mwenza wako..```

4. Nilikuwa nakuwaza
Ni muhimu kumjulisha mwenza wako kuwa unamuwaza hata kama hamko sehemu moja. Ukiona kitu kizuri au cha kuchekesha katika siku yako ambacho kinakufanya umkumbuke, mjulishe...```

5. Siku yako ilikuaje?
Muulize masuala ambayo mwenza wako anakutana nayo katika shughuli zake kazi kubwa waliyokuwa wakifanya. Kumpa nafasi mwenza wako kushare sehemu zingine za maisha yake kutasaidia kuumuweka sawa.```

6. Napenda mawazo yako.
Mwambie mwenza wako kuwa unapenda mawazo yake. Mjulishe kuwa unaona ana akili, mcheshi, anajua kupenda na ana kipaji.```

7. Nakuunga mkono
Mpe moyo mwenza wako kwa kumjulisha kuwa unaunga mkono maamuzi yake. Unaweza ukaenda mbali zaidi kwa kujaribu kumsaidia afanikishe malengo aliyojiwekea. Maisha yamejaa vikwazo vingi, na ile hisia kuwa una mtu mwingine upande wako zinaweza kukusaidia kuvivuka. Msiwe wanandoa tu, kuweni timu. Kumkumbusha mwenza wako kuwa upo nyuma yake kutaimarisha umoja wenu.

8. Hakuna kama wewe.
Mwenza wako anatakiwa kuwa rafiki yako. Kama hautaki kutembea naye, basi hamkupaswa kuwa pamoja. Mfanye mwenza wako ajue kuwa yeye ni bora na hakuna kama yeye.