Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa Tahadhari na angalizo la kuwepo kwa mvua kubwa leo Jumamosi January 22,2022 katika maeneo machache ya Mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Mbeya, Lindi, Mtwara pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba "athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi ya Watu kuzungukwa na maji na kusimama kwa shughuli za kiuchumi tuchukue tahadhari"