Maelfu ya raia nchini Ujerumani wameandamana katika wimbi la karibuni la maandamano ya kupinga vizuizi vya kupambana na COVID-19 pamoja na masharti ya chanjo. 

Jeshi la polisi limesema katika mji wa Freiburg waandamanaji karibu 4,500 tofauti na 7,000 waliotarajiwa waliandamana kupinga mapendekezo ya chanjo ya lazima na hatua nyingine za kukabiliana na janga hilo. 

Katika mji wa Leipzig mamia ya waandamanaji walijitokeza lakini maandamano hayo yalizimwa na polisi baada ya waandamanaji wachache kukiuka vizuizi vya polisi na wengine maelfu waliandamana kwenye maeneo mbalimbali ya jimbo la Saxony na miji mingine ya Ujerumani. 

Aidha maandamano kama hayo yalishuhudiwa katika mji mkuu wa Canada, Ottawa ambako maelfu waliingia mitaani kupinga ulazima wa chanjo, uvaaji wa wa barakoa na masharti ya chanjo.