Infinix inazidi kuwapa taharuki watumiaji wa simu za mkononi kwa kila toleo lake, imekua nikitu chakawaida kugusa kila mtu kwa muda mrefu tangu anzilishwaji wake. na kwa upande mwingine pia imekua ikiwapa ukakasi kampuni nyingine za simu kama samsung.

infinix hot 11 imekua ni mbadala wa Samsung A12 na imeteka soko kabisa wa toleo hilo la samsung kwa upande wa mtandaoni hadi kwa upande wa mauzo pia, hii nikwasababu ya sifa zifuatazo ambazo Infinix Hot 11 inazo kuzidi Samsung A12.

PLATFORM

Infinix Hot 11 inakuja na Os Android version ya 11 huku ikiwa na chipest ya mediatech helio ya G70 ambayo ina 12 nm pamoja na CPU yake ya Octa-core (2x2.0 GHz Cortex-A75 & 6x1.7 GHz Cortex-A55) na zaidi GPU ya Mali-G52 2EEMC2, huku ikiiacha mbali sana Samsung A12 kwani ina Os Android 10,ambayo wata i upgrade kwenye Android 11 kitu ambacho Infinix hot 11 imekuja nayo moja kwa moja.

CAMERA

Upande wa kamera pia kuna utofauti mkubwa sana kwani Hot 11 inakuja na kamera yenye uwezo wa 50MP kwa kamera ya nyuma ambayo ina uwezo mkubwa sana kwa toleo la hot pia kwa upande wa kampuni ya simu ya Infinix kwenye matoleo ya Hot hii ndio simu ya kwanza kuja na kamera kubwa huku ikiwa na feature ya Quad-LED flash, HDR, panorama na zaidi kwa upande wa video ni 1440p@30fps, kwa upande wa kamera ya mbele infinix hot 11 ina kamera moja yenye 8 MP, f/2.0, (wide) Dual-LED flash na video uwezo wake ni 1440p@30fps. huku upande wa samsung ina 48MP kwa kamera ya nyuma na uwezo wa video ni 1080p@30fps na upande wa camera ya mbele pia ina 8 MP, f/2.2 na video 1080p@30fps hiki pia ni chanzo kikubwa sana kwa wateja kuichagua na kuikimbilia infinix hot 11.

SAUTI

Matoleo ya Hot kwa upande wa infinix imekua ni matoleo ambayo yalikua special kwaajili ya mziki na sound kwa pamoja hivyo basi hata kwa upande huu imeweza kuitupa mkono A12 kutoka samsung kwani simu toleo hili Hot 11 kutoka infinix imekuja na speaker ambazo ni dual loudspeaker na 3.5mm jack kwaajili ya sauti nzuri na kuhakikisha mtumiaji anapata akitakacho kwenye simu yake. tofauti na Samsung A12 ina loudspeaker  ambayo ni speaker moja tu na pamoja ina 3.5mm jack ila kwa usikilizaji wa sound atakayo sikia mteja au mtumiaji wa Hot 11 na A12 itakua tofauti kwani simu hizi ni za vijana na vijana wanapenda mziki tena mziki mkubwa yaani loudspeaker ambao uta wasimamisha hisisa zao na hivyo wengi kukimbilia Infinix Hot 11 zaidi.

BETRI

Chaji imekua tatizo kwa baadhi ya makampuni ya simu mengi sana, na haswa kwa vijana wamekua wakilalamika sana simu kuto kukaa na chaji na zaidi wengi wamekua wakilalamika juu ya simu ku drain chaji kwa haraka zaidi na kuacha hali ya joto kali kipindi cha matumizi. Infinix Hot 11 inakuja na chaji ya 5200mAh ambayo ni Li-po pia ni betri ambayo haitoki huku Samsung A12 inakuja na betri ya 5000mAh na kwa matumizi ya vijana wengi wamekua wakipenda simu inayo weza kutunza chaji kwa muda mrefu na hivyo infinix hot 11 imeweza kuvutia na kuteka soko la vijana.

MEMORY

lengo la kampuni nyingi za simu ni kuhakikisha wateja wao wanapata kile wakitakacho kwa bei sahihi na kwa toleo sahihi, hivyo Infinix hot 11 ni simu kwaajili ya vijana haswa wanafunzi na imekuja na ukubwa wa kuhifadhi vitu wa 64GB 4GB RAM, 128GB 4GB RAM ambapo haihitaji gharama kubwa kwa kijana kumiliki simu yenye storage kubwa na mbadala kila kijana sasa anaweza kumiliki Infinix hot 11 na kupata akitakacho.

UPATIKANAJI

kwa upande wa upatikanaji simu za infinix zina patikana kwenye nchi zote za Africa na pia zaidi ukija Tanzania simu za infinix zinapatikana maduka yote ya simu ukifika ulizia simu ya kufunga mwaka 2021 unapewa infinix hot 11 au infinix hot 11 play uweze kufunga mwaka na simu janja kali kutoka infinix, samsung imekua ikiteua na kubagua baadhi ya mikoa kuto kupata au upatikanaji wake wa bidhaa hiyo unakua mgumu sana na hata wakati mwingine unakua wa gharama sana na hivyo kwa eneo hili tena Infinix imeweza kuteka soko kwa simu hii.

BEI

Simu matoleo ya vijana na bei zake pia ni kwa vijana na hatimae infinix imewafikia vijana wote na simu hii Inifnix Hot 11 inapatikana maduka yote kwa bei ya 400,000tsh tuu huku bei ya samsung A12 imekua ni ya juu kulinganisha na Infinix a12 inapatikana kwa 480,000 na kuendelea.

Endelea kutembelea page za zoom tech kwa taarifa za kila wakati na kupata ukitakacho kwa wakati na habari zote za tech