Na. John Mapepele
Waziri mwenye dhamana ya Michezo nchini. Mhe, Innocent Bashungwa leo Disemba 1, 2021 amewaongoza watanzania kuishangilia Timu ya Tanzania (Tembo Warriors) ambayo imefuzu na kuwa  timu ya kwanza miongoni mwa timu nne zinazoingia nusu fainali ya Soka ya Bara la Afrika kwa   wenye ulemavu (CANAF 2021) na hivyo kupata tiketi ya kushiriki  Mashindano ya Dunia  ya mchezo huo yatakayofanyika nchini Uturuki 2022 baada ya kuichapa timu ya Cameroon  mabao 5-0.

Timu ya Tanzania ambayo katika kipindi chote cha maandalizi imesimamiwa na  Kamati Maalum ya Kitaifa  chini ya Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassani Abbasi ilianza vizuri  kutokana hamasa  iliyotolewa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hasan.

Katika mechi zote za mashindano haya Tanzania imepoteza mechi moja tu ya Uganda mbayo ilifungwa goli 1-0, ambapo Tembo iliifunga timu ya Morocco 2-1 na Sierra Leone ambapo  tembo ilishinda  goli 1-0.


 Akizungumza na Waandishi wa Habari mara  baada ya mechi hii, Mhe. Bashungwa amewahakikishia kwamba Serikali itaendelea kuiisaidia  timu  hiyo ili iendelee  kufanya vizuri  maandalizi ya Kombe  la Dunia.

 Aidha, Dkt Abbasi amesema  kwa  kuwa  safari ya kuelekea  kombe la  dunia imekamilika kazi iliyobaki ni kuhakikisha kuwa  kombe  linabaki  Tanzania.

Magoli mawili ya Tanzania yamefungwa na  Alfan Kyanga dakika ya  2 na 15 , Ramadhan Chomole  dakika ya  18, na Frank Ngailo  dakika ya  36 na  44.

Mchezo huo pia umeshuhudiwa na  Rais wa Mashindano hayo duniani  Mateus Wildack.