Kundi la Taliban limetoa agizo la kupiga marufuku ndoa za lazima za wanawake katika kile kinaachonekana kuwa hatua ya kushughulikia vigezo viliyowekwa na mataifa yaliyoendelea kama sharti la kuitambua serikali yao na kurejesha misaada. 

Kiongozi Mkuu wa Taliban,Hibatullah Akhunzada ametangaza hatua hii wakati Afghanistan ikigubikwa na umaskini tangu Taliban walipochukua madaraka mnamo Agosti mwaka huu. 

Uongozi wa Taliban umesema umeamuru mahakama za Afghanistan kushughulikia haki za wanawake hasa wajane wanaotafuta urithi wa jamaa zao wa karibu. 

Ndoa za lazima zimekuwa jambo la kawaida nchi humo, wakati wakimbizi wa ndani wanawaozesha mabinti zao wadogo kwa mahari ambayo inaweza kutumika kulipa madeni na kulisha familia zao.