KUPATIKANA NA BHANGI NA POMBE MOSHI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mwanamke mmoja aitwaye ELIZABETH AGUSTINO CHATANDA [30] Mkazi wa Kyela Kati akiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi na Pombe ya Moshi @ Gongo nyumbani kwake.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 23.12.2021 majira ya saa 23:30 usiku katika msako uliofanyika huko Kitongoji cha Kyela Kati, Kata ya Ndandalo, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Baada ya kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake alikutwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi Kete 41 pamoja na Pombe Moshi @ Gongo lita 24 iliyokuwa imehifadhiwa kwenye chupa ndogo 48 tayari kwa ajili ya kuuzwa. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa shauri hili kukamilika.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA MATUKIO YA KUVUNJA NYUMBA USIKU/MCHANA NA KUIBA.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia 1. WILLIAM SANGA [25] Mkazi wa Tukuyu 2. STAMILI HEMED [25] Mkazi wa Mikoroshini 3. SAMSON RINGSON KYANDO [27] Mkazi wa Mikoroshini na 4. FREISON SAMSON MBILINYI [52] Mkazi wa Kyela Kati kwa tuhuma za matukio ya kuvunja nyumba usiku/mchana na kuiba.

Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 23.12.2021 katika msako wa pamoja uliofanyika Wilaya ya Rungwe na Kyela mkoani Mbeya na katika upekuzi uliofanyika kwenye makazi yao walikutwa na mali mbalimbali za wizi ambazo ni:-

  1. Radio Subwoofer aina ya Sea Piano mbili.
  2. Television Flat Screen aina ya EVVOLi inchi 21.
  3. Television Flat Screen aina ya Aborder inchi 17.

Mtuhumiwa WILLIAM SANGA baada ya kuhojiwa alikiri mali hizo aliiba Wilaya ya Rungwe na kwenda kuuza Wilaya ya Kyela kwa kushirikiana na watuhumiwa wengine. Watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa makosa ya kuvunja nyumba usiku/mchana na kuiba.

KUINGIA NCHNI BILA KIBALI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia BARAKA TADESA [19] raia wa nchini Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 23.12.2021 majira ya saa 22:00 usiku huko katika kizuizi cha Polisi Kayuki kilichopo Kijiji cha Kayuki, Kata ya Ilima, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa alikuwa akisafiriki kutoka Kenya kuelekea Afrika Kusini akitumia gari namba T.933 CJC Toyota Carina. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendesha msako wa kumtafuta dereva wa Gari hilo ambaye alikimbia na kulitelekeza Gari hilo baada ya kuwaona askari Polisi.