Kukosa choo ni tatizo kubwa katika jamii zetu japo huwa halionekani kama ni tatizo. Hata hivyo kuna vyakula ambavyo vinapatikana kwa urahisi na vinasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa njia rahisi kabisa.

Kwa kawaida mtu mwenye afya njema anatakiwa kwenda chooni angalau mara tatu kwa siku,  lakini si ajabu kusikia mtu hajaenda chooni siku tatu na tunaona ni kawaida sana kwenda chooni mara moja kwa siku.

Vifutavyo ndivyo vyakula ambavyo husaidia kutibu tatizo la kukosa choo.

Tende
Tende zikiwa kavu au kama juisi inasaidia kuondoa tatizo la kukosa choo. Tende zina fiba kwa wingi hivyo kusaidia zoezi la usagaji chakula tumboni. Pia Tende zina kemikali ya sorbitol–aina ya sukari ambayo inatajwa kusaidia usagaji chakula.

Maji
Kunywa maji kwa wing kunasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa kuwa maji yanahochea usagaji wa chakula na kufanya choo kuwa laini.

Wataalamu wa afya wanashauri kunywa glasi 6 mpaka 8 za maji kila siku( Lita 1-2 kwa siku)

Ulaji wa Matunda au Saladi
Matunda yanasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa vile yana fiba kwa wingi. Lakini matunda yanasaidia kuongeza maji maji hasa matunda kama matikiti.

Ulaji wa Mboga za Majani
Mboga za majani kama ilivyo matunda ni chanzo kizuri cha faiba ambazo ni muhimu sana katika usagazi na usukumaji wa chakula.

Mchicha, Spinachi,karoti na mboga mboga nyingine ni muhimu kuwepo katika chakula cha kila siku.

Mazoezi
Ukiachia vyakula,ufanyaji mazoezi au kazi zinazoshughulisha mwili zinazaidia kuzuia na kutibu tatizo la kukosa choo.

Kufanya mazoezi kila siku angalau kwa dakika 30 ni jambo linalowezekana kama utalipa muda na kuweka katika ratiba zako. Mazoezi rahisi kabisa ni kukimbia (jogging) na pia hushughulisha mwili mzima(Total Body Exercise).

Ukiachia kutibu tatizo la kukosa choo pia mazoezi yanasaidia kuzuia magonjwa mengine mengi kama presha na kisukari.