"Duniani huko kumeanza wimbi la nne la Covid 19 hatuna budi kuchukua kila tahadhari, tumeleta chanjo nendeni mkachanje, jambo hili hatuwezi jua lini litafika kwetu maana tunasafiri na kwa wenzetu limeanza basi tuchukue tahadhari hilo wimbi la nne hata likifika lifike likiwa na kasi ndogo ya vifo na maambukizi"

"Kwasababu Balozi wa Japan yupo hapa nishukuru sana utamaduni wa Japan, Wenzetu Wajapan ni utamaduni zao siku zote wakisalimiana hawapeani mikono wanafunga mikono na kuinama na ndio utamaduni walioturithisha katika janga la Covid kwahiyo sio lazima tupeane mikono tufunge mikono tusalimiane" ——— Rais Samia akifungua Barabara ya Morocco - Mwenge (KM 4.3)