Rais Samia Suluhu Hassan amepeleka ujumbe wa tahadhari kwa Waziri wake wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa kufuatia msururu wa madudu unaoendelea katika taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.
Amemtaka Waziri Mbarawa afanye marekebesho yanayowezekana ndani ya wizara yake ili mambo yaendelee kufuatia uwepo wa ubadhirifu mkubwa katika bandari ya Dar es Salaam.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 4, 2021, jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa gati 0 hadi 7 ya Bandari ya Dar es Salaam.
"Mh. Waziri nilikuweka kwa kukuamini na ninaomba nenda kasimamie kazi hii kama ninavyotarajia na utakaposhindwa njoo uniambie, nimeshindwa, nitaangalia mwingine labda ataweza kunisaidia, lakini haya hayawezi kuendelea," amesema Rais Samia.
==>>Msikilize Hapo Chini