Mwanamuziki Mkongwe wa Rhumba kutoka Congo, Francoise Lulendo Matumona maarufu General Defao amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi nchini Cameroon alikokwenda kutumbuiza

Defao alijizolea umaarufu mkubwa kwa miondoko yake ya Ndombolo and Ekibinda Nkoi.

Defao alizaliwa Desemba 3, 1958 Kinshasa nchini Congo ni mwanamuziki mwenye uwezo wa kutunga nyimbo na kuimba na kucheza muziki.

Familia imethibitisha kifo cha mwanamuziki huyo aliyefariki nchini humo alipokwenda kwa ajili ya kutumbuiza kipindi cha sikukuu.