Nguli wa muziki wa Rumba kutoka Congo, Général Defao (63) amefariki dunia nchini Cameroon alikokwenda kutumbuiza.

Defao ambaye jina lake ni Lulendo Matumona alitambulika rasmi kwenye muziki mwaka 1976, akatoa nyimbo kubwa kama Sidewalk radio, Kikuta family na School love.