Mbunge wa Geita vijijini Joseph Kasheku Msukuma ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima PHD ya Siasa na Uongozi kutoka chuo cha The American Univercity USA cha nchini Marekani.

Msukuma na wenzake 15 akiwemo mwanaharakati Frola Lauo wa Nitetee Foundation aliyetunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima wa Falsafa mwingine ni aliyewahikuwa Waziri wa Kilimo ambaye ni Mbunge wa Vwawa Songwe Japhet Hasunga.

Shahada hizo wametunukiwa mkoani Dodoma na Profesa Madhu Krishan mwakirlshi wa chuo hicho.

Msukuma mwenye elimu ya darasa la saba amesema chuo hicho kimemfuatilia kwa kipindi cha miaka mitatu katika michango yake bungeni kupitia video za YOUTUBE na alikuwa akipigiwa simu mara kwa mara kwaajili ya kumfuatilia mpaka Desemba 5,2021 ambapo ametunukiwa heshima hiyo.