Wakati kirusi kipya cha corona kiitwacho Omicron kikiendelea kuipasua kichwa dunia, Ligi kuu ya England imefuta mechi kadhaa kutokana na ongezeko la maambukizi ya kirusi hicho ambapo hadi sasa Wachezaji wengi wamejiweka karantini huku mechi zikiahirishwa ikiwemo ya leo ya Leeds United vs Aston Villa ikikumbukwa pia kwamba Leeds vs Liverpool iliyopangwa kuchezwa juzi nayo iliahirishwa.

Game ya Wolves vs Arsenal pia haitochezwa leo ambapo Wolves iliomba isogezwe mbele kwa sababu haina idadi ya kutosha ya Wachezaji kutokana na wengi kupatwa na covid 19, vilevile mechi ya Wolves vs Watford iliahirishwa hiyo jana na kufanya jumla ya mechi za Premier League zilizoahirishwa kufikia 15 katika kipindi cha wiki mbili na nusu zilizopita kisa kikiwa ni corona.

Mparanganyo huu umeibua mjadala wa kuruhusiwa kutumika kwa Wachezaji watano wa akiba badala ya watatu kama ilivyo kwa sasa huku Makocha wengi wakipaza sauti zao akiwemo Thomas Tuchel, Patrick Vierra, Ralf Rangnick na Pep Guardiola wa Man City.