Hakuna jambo rahisi zaidi katika maswala ya kutongoza mwanamke kama kuchukua namba yake ya simu. Unaweza ukaongea kwa nusu saa na yeye kisha ukamwomba namba yake ya simu na akakupatia.

Lakini wanaume wengi shida yao ni woga wa kumuaproach mwanamke kuwapatia namba wao wenyewe. Mara nyingi utapata wanaume wakiomba marafiki zao namba za wanawake. Haya ni makosa makubwa kwa kuwa nafasi zako za kumuwini mwanamke kama huyu zinapungua.

Ukiomba namba ya simu ya mwanamke kupitia kwa marafiki zako, utakuwa na maswali mengi ya kujibu kwani wanawake hawapendi kupeana namba zao za simu na mara nyingi utapata maswali kama vile, "namba yangu umeitoa wapi?'

Ili kuepuka changamoto kama hizi, Hizi hapa ni mbinu rahisi za kutumia kupata namba ya simu kutoka kwa mwanamke.

Mpe muda wote aongee.
Hakikisha unamwangalia machoni mwake wakati wote anapokuwa akiongea na umakinike kwa kumsikiliza kila atakachoongea. Yachukue maneno yake yote na uweke hisia zako vile inavyotakiwa. 

Jambo muhimu linalotakiwa hapa ni kuhakikisha kuwa unampa nafasi aongee kila kitu anachotaka yeye bila hivyo ataona kuwa msingi wako na yeye haufai ama kutokuwa na maana. Kama ni mwanamke asiyependa kuongea sana basi makinika na ishara zake anazozifanya na pia miondoko ya macho yake.

Msikilize kwa umakini.
Hakikisha umemakinika wakati wote mnapokuwa mnaongea, na kuchukua baadhi ya maneno anayoongea ili uweze kuyapanua baadae katika maongezi yenu. 

Ukimakinika zaidi kunasaidia kwa sababu kutatoa fursa ya kuleta maongezi ambayo yanahusiana na yakuvutia ambayo yatampendeza huyo mwanamke. 

Fahamu ya kuwa wakati mwanamke anapoongea ama kutoa stori yake, ni dhahiri kuwa wakati mmoja au mwingine mnaweza kuwa na mfanano wa matukio yanayohusiana so ni vyema kumakinika ili kuweza kujenga stori za pamoja. 

Hii itakusaidia wewe kuweza kumfanya mwanamke kukupenda na kukuamini. Atakupenda kwa urahisi bila hata wewe kutokwa na kijasho.

Muulizie namba yake.
kama hutaki kuchukua hatua zaidi yapo, then unahitajika kumwomba namba yake finally. Hii itakuja automatically yenyewe wakati umemaliza na kutimiza hatua ya kwanza na ya pili bila wasiwasi. 

Hii haiwezi kuwa tatizo kwani tayari ushajenga msingi ambao unamfanya mwanamke akupende.
Kama unashindwa utatumia ujuzi gani wa urahisi kuomba namba yake basi fanya hivi. 

Katika hatua ya kwanza na ya pili ya maujanja haya, itakuwa tayari ushafahamu mengi kumhusu huyu mwanamke so unaweza kuleta issue moja ambayo ashawahi kuitaja wakati flani. Mfano kama ashawahi kutaja anapenda kutembea then mwambie "Naona tunafaa siku moja tutembee pamoja". 

Wakati mwingine mwanamke anaweza kuanzisha swala kama hili wa kwanza, so akikubali unamwomba namba yake fasta. Hawezi kukunyima.

So kama kweli wataka kujua kuchukua namba kutoka kwa mwanamke, achana na porojo na mbinu wasiwasi za marafiki zako wanazozitumia ambazo mara nyingi hazifaulu. 

Pia sahau zile mbinu zote unaziona katika sinema. Kando na kuwa mwanamke anaweza kukupenda, lazima ujenge msingi ambao utamfanya mwanamke yeyote kujiskia huru na wewe -jambo ambalo wanaume wengi hukosea kufanya.