Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameionya Urusi kuwa, italipa gharama kubwa iwapo, itaivamia Ukraine. Blinken ameitaka Moscow kutumia njia za kidiplomasia kutatatua changamoto zozote na Kiev.

"Hatima  ipo mikonini mwa urusi iache kuchochea wasiwasi unaoendelea kwa kuacha mazoezi ya kijeshi na kuacha kutisha Ukrane, tunaangalia kinachoendelea kwa karibu na tunawasiliana na kushrikiana na washirka wetu"-Amesema.

Blinken ametoa kauli hii, baada ya kuzungumza na mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov jijini Stockholm nchini Sweden huku Bw. Lavrov akisema Urusi haina mpango wa kupigana na Ukraine.

Onyo hili linatolewa siku moja baada ya Washington kusema iko tayari kujibu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, ikiwa ni pamoja na kuiwekea vikwazo.