Maafisa wanaosimamia uchaguzi wa kwanza wa rais katika nchi iliyoharibiwa kwa vita ya Libya wamethibitisha kuwa haiwezekani kuandaa uchaguzi huo Ijumaa hii kama ilivyopangwa na kupendekeza uahirishwe kwa mwezi mmoja. 

Uchaguzi huo ulikusudia kuleta mwanzo mpya katika taifa hilo la Afrika Kaskazini, mwaka mmoja baada ya muafaka wa kihistoria wa kusitisha vita na zaidi ya muongo mmoja baada ya vuguvugu la mapinduzi yaliyomuondoa madarakani na kumuuwa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.

Siku ya jana mwenyekiti wa kamati ya bunge inayofuatilia uchaguzi huo imemwambia spika wa bunge kuwa baada ya kutathmini ripoti za kiufundi, mahakama na usalama, haitowezekana kuandaa uchaguzi huo Desemba 24. Haikupendekeza tarehe mbadala ya kupigwa kura hiyo, lakini tume ya uchaguzi ya Libya imependekeza usogezwe hadi Januari 24.