Kenya: Watu 20 wafariki dunia katika basi lililosombwa na mto
Zaidi ya watu 20 wamefariki dunia Jumamosi Desemba 4 wakati basi lao lililokuwa likielekea kwenye harusi liliposombwa na Mto Enziu uliofurika maji kwenye daraja moja katikati mwa Kenya, polisi imesema.
Wapita njia wamepiga kelele wakati basi la shule ya manjano lililokodiwa kusafirisha wanakwaya ya kanisa na wengine kwenye hafla iliyopangwa katika Kaunti ya Kitui lilipinduka na kuzama dereva akijaribu kujaribu kuongoza basi lake kwenye kinakirefu cha maji.
Baadhi ya watu waliokuwa kwenye basi hilo walifanikiwa kujiokoa kabla ya basi kuzama katika maji na kupelekwa mahali salama. "Tulipata ajali hii mbaya iliyotokea hapa asubuhi ya leo," gavana wa Kitui Charity Ngilu amewaambia wanahabari.
Ameongeza kuwa "miili 23" hadi sasa ilikuwa imetolewa mtoni na "bado kuna miili kwenye basi". Amesema shughuli ya kuitafuta miili ya waathiriwa itaanza tena leo Jumapili a
Basi hilo lilikuwa likiwasafirisha wakwaya wa kanisa na wanakijiji waliokuwa wakkenda harusini wakati wa ajali hiyo. Walioshuhudia wamesema kuwa dereva wa basi hilo alijaribu kuvuka daraja, huku likiwa limefurika kwa maji, ambayo nguvu yake ilisomba gari hilo katika mkondo wa mzunguko. Makamu wa Rais William Ruto ametoa rambirambi zake kwa familia za waathiriwa, huku akiwataka madereva wa magari kuchukua tahadhari zaidi katika barabara za Kenya, ambako maeneo mengi kwa sasa yanakumbwa na mvua kubwa