Kampuni ya simu Infinix rasmi Infinix NOTE 11 na Infinix NOTE 11 pro mwanzoni mwa mwezi Octoba huko Ugaibuni. Infinix NOTE 11 pro ni simu ya kwanza kwa kampuni ya simu Infinix kuja na Gaming processor ya MediaTek Helio G96 na refresh rate ya 120Hz. 


Kulingana na uchambuzi uliofanywa na blog kuwa ya tech duniani ‘Gadgets’ https://gadgets.ndtv.com/mobiles/news/infinix-note-11-pro-launch-price-specifications-mediatek-helio-g96-soc-5000mah-battery-2576238ni dhahiri Infinix NOTE 11 pro ni simu ambayo inaweza kufanya kile ambacho computer ingefanya kwa speed ile ile.


Kupitia mifano mbalimbali ya simu za awali za Infinix inasemekana Infinix NOTE 11 pro si kwamba tu ni simu ya kwanza kuja kuwa na speed kubwa zaidi wa ufanyaji kazi za kiofisi na kucheza games za ujazo mkubwa kwa muda mrefu pasipo simu kupata moto lakini pia itakuwa simu ya kwanza ya series ya NOTE kuwa na kioo chenye refresh rate ya haraka zaidi na kumfanya mtumiaji afurahie wakati wa kuperuzi application mbalimbali.


Ukichungulia page ya instagram ya @infinixmobiletz unaona ni namna gani simu hii imeweza kuzua taharuki idadi kubwa ikitamani kujua bei ya simu hiyo fununua zinadai kuwa Infinix NOTE 11 pro itapatikana kwa bei rafiki kabisa ya sh. 600,000 za Kitanzania lakini kwa mteja wa pre-order atapewa punguzo la sh.50,000  https://www.instagram.com/p/CVcq1X7td2Y/.


Kaa tayari kupokea mzigo huu nchini Tanzania mwishoni mwa mwezi Octoba.