Bei ya Petrol,Dizeli, Mafuta Ya Taa Yazidi Kupanda
Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) imetangaza kupanda kwa bei ya rejareja ya mafuta kwa Sh71 kwa lita moja ya petroli mwezi huu.
Tangazo la Ewura lililotolewa linaonyesha kupanda kwa viwango tofauti kwa bei ya petroli, dizeli na mafuta ya taa ikilinganishwa na mwezi uliopita.