Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amefanya mabadiliko kwa kuwaondoa watumishi sita katika nyadhifa zao kwa sababu mbalimbali za utendaji  uliosababisha kuzorota kwa   huduma ya maji Wilaya ya Newala na Nanyamba mkoani Mtwara.

Walioondolewa ni mhandisi Primy  Shirima (meneja wa Ruwasa mkoa), mhandisi Rejea Ng’ondya (mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi Mtwara-Mtuwasa), mkemia Alualus Mkula (mkuu wa maabara ya ubora wa maji mkoa), mhandisi Emanuel Konkomo (mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Makonde), mhandisi Renard Baseki (meneja wa Ruwasa- Newala) na Anza  Makala (mkuu wa kitengo cha manunuzi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Makonde).

Imeelezwa kuwa wataalam hao wa sekta ya maji watapangiwa majukumu mengine na wizara.