Watu tisa wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya hiace ya kubeba magazeti iliyokuwa ikitoka jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Desemba 13, 2021 alfajiri katika kijiji cha Mahenge wilayani Kilolo mkoani Iringa.

Kamanda Bukumbi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo gari hilo lilimshinda dereva kwenye kona na kugonga mti uliokuwa pembezoni mwa barabara na kupinduka na kusababisha vifo vya watu 9.

“Watu 9 wamepoteza maisha katika ajali hiyo ambapo wanawake 4 wanaume 5 na majeruhi watatu wanaendelea kupewa matibabu katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa” Kamanda Bukumbi