Watu watano wa familia moja wamefariki dunia, baada ya nyumba waliokuwa wakiishi kuteketea kwa moto wakati wakiwa wamelala usiku wa kuamkia Novemba 08, 2021.

Tukio hilo limetokea katika mtaa wa Igoma Mashariki kata ya Igoma wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza na kuteketeza kila kitu katika nyumba hiyo wakiwamo watu hao.

Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mwanza, Ambwene Mwakibete amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya Moto na kusema kuwa waliofariki ni watu wa familia moja.

“Ni kweli waliofariki ndani ni Lameck Benedicto, mke wake, mtoto wake wa kike na wageni wake wawili ambao bado majina yao hayajatambulika,”.