Watu 115 waliofariki kwenye mlipuko wa gari la mafuta Ijumaa ya Wiki iliyopita, nchini Sierra Leone wamezikwa kwa pamoja katika Mji Mkuu wa Nchi hiyo wa Freetown huku wengi wakiwa wameungua sana hadi kushindwa kutambulika kwa urahisi.

Rais wa Nchi hiyo, Julius Maada Bio ametangaza siku tatu za maombolezo na bendera zinapepea nusu mlingoti kufuatia janga hilo, Serikali kupitia Wizara ya Afya imethibitisha kuwa hadi sasa wamefariki Watu 115 lakini wengine zaidi ya 100 bado wamelazwa Hospitali wakitibiwa majeraha.