Watoto watatu wa Famila moja katika Kijiji cha Ngecha Kaunti ya Kiambu nchini Kenya wamefariki kwa kuungua moto wakiwa wamefungiwa ndani na Mama yao Lucy Wambui (32) ambaye alikwenda dukani kununua maharage na mahindi.

Watoto hao ambao mmoja anaitwa Brandon Kiriro (5), Donnel Kinuthia (2) na Nellan Wanjiru mwenye umri wa miezi 10 wamefariki baada ya nyumba waliyokuwemo kuwaka moto unaodaiwa ulitokana na moto wa mshumaa waliokuwa wanautumia.

Ripoti zinasema Mama aliporudi kutoka dukani na kukuta nyumba inaungua aliwaambia majirani kuwa ndani kuna Watoto lakini walikuwa wameshachelewa na wote wakafariki, Mama alipelekwa Hospitali baada ya kupata mshtuko lakini anaendea vizuri.

Kufuatia tukio hilo Polisi Katika eneo hilo wamewaasa Wazazi au Walezi wenye tabia ya kuwafungia Watoto ndani na kwenda umbali mrefu kutafuta mahitaji au kufanya shughuli nyingine mbalimbali , kuzidisha umakini ili kuepusha majanga.