TANGAZO LA USALIMISHAJI WA SILAHA KWA HIARI.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ULRICH MATEI anapenda kuwatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Mbeya kuwa zoezi la kusalimisha silaha kwa hiari limeanza tangu tarehe 01 Novemba, 2021 na litafanyika hadi tarehe 30 Novemba, 2021 kwa kuzingatia tangazo la serikali namba 774 la tarehe 29 Oktoba, 2021 lililotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.GEORGE SIMBACHAWENE.

Silaha hizo zitasalimishwa katika vituo vya Polisi, Ofisi za serikali za mitaa na ofisi za watendaji wa Kata kila siku kuanzia majira ya saa 02:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.

Mtu yeyote ambaye anamiliki silaha kinyume cha sheria ikiwa atasalimisha silaha hiyo katika kipindi kilichotangazwa atapewa msamaha na hatashitakiwa kutokana na uamuzi wake wa kusalimisha silaha hiyo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa wananchi wote wa mkoa wa Mbeya kwa yeyote anayemiliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha kwa hiari katika maeneo yaliyotajwa.

Aidha kwa yeyote anayemiliki silaha ya mtu aliyefariki au aliyepoteza sifa za kumiliki silaha hiyo afike kituo cha Polisi kwa ajili ya kufuata taratibu za kisheria na kuomba kumiliki silaha hiyo kihalali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya anatoa rai kwa viongozi wote wa serikali, viongozi wa dini zote, viongozi wa mila, machifu, MUJATA, wazee mashuhuri, viongozi wa kisiasa kwa ujumla wao wakiongozwa na viongozi wa chama cha mapinduzi kutoa ushirikiano wa dhati kwa mustakabali wa amani ya nchi yetu.

Mara baada ya muda uliotangazwa kupita, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama, viongozi wa serikali za mitaa na kata litaendesha msako mkali nyumba kwa nyumba dhidi ya mtu/watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na hatua kali za kisheria zitachukuliwe dhidi ya yeyote atakayekamatwa anamiliki silaha kinyume cha sheria.
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.