Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amesema wanafunzi 4,188 sawa na asilimia 0.46 wamechaguliwa kujiunga na shule za bweni za Kitaifa.

Akitangaza upangaji wa wanafunzi hao Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu amesema nafasi zinazokwenda kwa wanafunzi wa bweni ni za shule za Kitaifa huku nafasi nyingi zikiangukia zaidi kwa wanafunzi wa vijijini.

Akizungumzia kigezo, Ummy amesema kuchagua wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Kwanza kumezingatia mwanafunzi kufikisha jumla ya alama za ufaulu kuanzia 121 hadi 300 kati ya alama 300.

Ameongeza mgawanyo wa wanafunzi kwa shule za bweni zenye ufaulu mzuri na zile za bweni ufundi zimegawanywa kwa kila Mkoa kulingana na idadi ya watahiniwa waliosajiliwa katika Mkoa husika kwa kutumia Kanuni ya kugawa nafasi hizo kitaifa.


_______

 

Amefafanua Shule za Sekondari za Bweni za kitaifa za Kawaida, zimegawanywa kwa kila Halmashauri kwa kufuata idadi ya watahiniwa waliotoka katika mazingira magumu tu kwa kutumia Kanuni ya kugawa nafasi hizo kitaifa.

"Wanafunzi waliopangiwa shule za bweni za Kitaifa ni 1989 na hapa tumechukua zaidi wanafunzi wa Vijijini lakini kwenye majiji na halmashauri tumeangalia sana wenye uhitaji tu,"

Aliongeza Wanafunzi 934 ikiwa wavulana 514 na Wasichana 420 sawa na asilimia 0.1 wamechaguliwa kujiunga na Shule za Sekondari za wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi.

Huku wanafunzi 1,265, wavulana wakiwa ni 1,070 na Wasichana 195 sawa na asilimia 0.14 wakichaguliwa kwenda Shule za Sekondari za Ufundi.

Amesema wanafunzi 1,989, wavulana wakiwa ni 1,036 na wasichana 953 sawa na asilimia 0.22 wamechaguli.


_______