Mwigizaji Staa wa Marekani Vin Diesel (54) amemtaka Mwigizaji mwenzie Dwayne Johnson "The Rock", kumaliza kile kinachotangazwa kama kuna ugomvi kati yao na kumtaka warudi tena kuungana ili wamalizie "Fast & Furious 10" pamoja .

Vin Diesel ameandika barua fupi ya wazi kupitia akaunti yake ya Instagram akielezea ukaribu waliokuwa nao hata kwa Familia zao na kumwambia Dunia inasubiri Fast & Furios 10, "Mdogo wangu Dwayne muda umefika Dunia inasubiria Fast & Furios 10, naapa kwamba lazima niikamilishe Fast & Furios 10 lakini unapaswa kuwepo pia una kazi kubwa ya kufanya kwenye hii"