VIDEO: Majibu ya serikali kuhusu utaratibu wa uuzaji Makinikia
Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema kilichofanyika kwenye uuzaji wa makinikia ya madini nchini ni kubadili mfumo wa uuzaji rasilimali hiyo.
Amesema kuwa utaratibu wa awali ulikuwa unamruhusu mwekezaji kusafirisha mchanga huo nje ya nchi, na baada ya kuchenjuliwa ndipo anarudi nchini kusema madini aliyoyapata, kisha anauziwa.
Amefafanua zaidi kwamba, mfumo wa sasa serikali inapima madini yaliyopo kwenye mchanga huo kwa kutumia maabara tatu tofauti za timu za watu wasiofahamiana, na baada ya hapo wanauza mchanga huo kama madini.
Msikilize Waziri Biteko hapa chini akitolea ufafanuzi suala hilo wakati akiwasilisha tathmini ya mwenendo wa wizara kuelekea miaka 60 ya uhuru.