Uholanzi imeanza kuwapeleka wagonjwa wa Covid 19 nchini Ujerumani kutibiwa ili kupunguza shinikizo kubwa linalozizonga hospitali za nchi hiyo zilizoko katika hali mbaya ya kukabiliana na ongezeko la wagonjwa walioambukizwa virusi vya corona. 

Jumanne mgonjwa mmoja alisafirishwa kwa gari la wagonjwa kutoka mji wa Rotterdam na kupelekwa hospitali ya Bochum, Ujerumani, iliyoko kiasi kilomita 240 mashariki mwa nchi hiyo, na mgonjwa mwingine alisafirishwa baadaye. 

Idadi ya wagonjwa wa Covid-19 katika hospitali za Uholanzi imeongezeka na kufikia kiwango kikubwa sana katika kipindi cha wiki za karibuni ambacho hakijawahi kuonekana tangu mwezi Mei. 

Hospitali za Ujerumani zimeweka vitanda jumla ya 20 kwa ajili ya wagonjwa kutoka Uholanzi.