Tumieni Sekratarieti Za Mikoa Ipasavyo Kufanikisha Zoezi La Anwani Za Makazi
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala A Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy ameishauri Wizara ya Habari, Mawasiliano na Tekinolojia kuzitumia Sekretarieti za Mikoa ili kufanikisha zoezi la Anuwani za Makazi kwa kuhakikisha pia wanazitengea bajeti ya ufuatiliaji ili kuharakisha utekelezaji wa mfumo wa Anwani za Makazi katika maeneo yao.
“Mhe Ummy amesema Sekta ya afya, wamekuwa wakitenga kiasi, sekta ya elimu wanafanya hivyo, na wizara ya Mawasiliano muangalie namna ya kutenga fedha za ufuatiliaji wa mradi huu”
Akizungumza kwenye semina ya Wakuu wa mikoa 26 ya Tanzania Bara iliyolenga kuwawapa uwelewa wa namna ya kutekeleza Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi, Mhe. Ummy alisema Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeweka mikakati ya kuipanga, na kuiendeleza miji ikiwamo inayochipukia na kuwa mfumo wa anwani na Makazi pia utasaidia kufikia azima hiyo.
Aidha, Mhe. Ummy amesema kunafaida nyingi kutekeleza Mfumo wa Anwani za makazi ikiwamo usalama.
” Jambo la anwani za makazi ni zuri sana hususani katika miji yetu na mimi binafsi nimelipa kipaumbele suala zima la uendelezaji miji na vijiji.”
Kwa upande wa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari, Dk Ashatu Kijaji amesema mkakati uliopo ni kuhakikisha asilimia 75 ya Watanzania wanafikiwa na huduma ya anuwani ya makazi ifikapo Aprili mwakani.