Kampuni ya simu za mikononi TECNO imezindua rasmi toleo jipya la simu ya CAMON 18 Series jana katika fukwe za hotel ya Sea Cliff Dar es Salaam.

 Uzinduzi huo ulihudhuliwa na watu maarufu mbalimbali ikiwepo muigizaji maarufu Tanzania Elizabeth Michael ama wengi wanamfaham kwa jina la uigizaji “Lulu”, mpiga picha maarufu Bernard Atilio na mlimbwende Jihan Dimack nao waliudhuria hafla hio. Makampuni makubwa nchini  Vodacom na Air Tanzania waliudhuria hafla hio wakiwa kama washirika wakuu kwenye uzinduzi huo.
 


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, mkufunzi wa kampuni hiyo Ms. Shakila Mkima amesema “simu hiyo imeboreshwa zaidi kwenye upande wa kamera na Processor, ambapo simu hiyo ina teknolojia ya kisasa kwenye upande wa kamera iitwayo GIMBAL CAMERA. Ambapo itamsadia mtumiaji kushoot video bila kutisika au kucheza cheza. Ukiondoa sifa hiyo pia CAMON18 ina uwezo wa kuzoom mara 60x zaidi.


Pamoja na kuwa na kamera kubwa yenye uwezo, pia simu ya TECNO CAMON  18  ina memori kubwa inayofikia GB 256 ROM kwa GB 8 RAM. Ukubwa wa memori ya simu hii utamsaidia mtumiaji kuhifadhi vitu vyake bila kufuta pia kuiwezesha simu kufanya kazi kwa ufanisi zaidi bila kukwamakwama.

 TECNO imeingia ubia na washirika wakubwa kwaajli ya kumjali mteja atakae nunua CAMON 18 washirika hao wakiwa ni AIR Tanzania ikitoa safari yam waka mzima bure Pamoja na VODACOM ikitoa kifurushi cha Mwaka mzima ikiwemo Muda wa maongezi, SMS na Internet bure, kwa Pamoja wakizindua kampeni iitwayo “RUKA NAYO”