Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) na Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi katika taasisi tajwa hapo juu kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 04 – 06 Desemba, 2021 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili utafanyika kuanzia tarehe 04 – 06 Desemba, 2021 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;
ii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask);
iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;