Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesaini mkataba wa USD Milioni ( Tsh. Bilioni 69.1) kwaajili ya kuboresha huduma za kimtandao na kampuni ya India Tech Mahindra .
Akizungumza wakati wa kutia siani katika Ofisi za Makao Makuu ya TANESCO mkoani Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande amesema kampuni hiyo imeshinda kandarasi hiyo na mfumo huo utasaidia kubaini athari wanazokutana nazo wateja na wafanyakazi na kutatua kwa haraka.
“Mfumo huu moja ya sehemu ni kuongeza ufanisi katika huduma kwa wateja ile call center itasaidia kujua matatizo ya wateja kwa urahisi na ukiwa na tatizo la umeme mfano mteja akawa sehemu anahitaji kufungiwa umeme na mita hakuna sisi kama viongozi tutajua na kutatua”
“Mfumo huu muda wake ni miezi 30 na matokeo yataanza kwa miezi 12 ya mwanzo na mpaka kukamilika ni miezi 30". Maharage