Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania umewakumbusha Raia wote wa kigeni ambao ni Watu wazima wataosafiri kwenda Marekani kwa njia ya anga kuanzia Jumatatu ijayo tarehe 8 November watatakiwa kuonesha uthibitisho kuwa wamepata chanjo kamili ya covid 19.

Pamoja na hilo pia atatakiwa kuonesha cheti kinachoonesha kwamba hana maambukizi ya covid 19 baada ya kufanya kipimo ndani ya siku tatu zilizopita.


Taarifa ya Ubalozi imesema “Raia wa Marekani waliopata chanjo na Wakaazi wanaorudi Marekani watahitaji kuwa na cheti kinachoonesha hawajaambukizwa covid 19, pia Raia na Wakaazi ambao hawajapata chanjo watahitaji kuwa na cheti kuonesha hawana maambukizi kutokana na kipimo kilichofanyika siku moja kabla ya safari”