Kampuni ya simu Infinix imekuwa kileleni kwenye biashara ya simu tangu kuzinduliwa kwake Tanzania. kupitia simu za Infinix tumeona teknolojia mpya na hii inapelekea kuwa na shahuku kubwa tangu Infinix kuanza kutupia mtandaoni simu aina ya Infinix NOTE 11 na NOTE 11 pro na kudai hizi ndio simu za kwanza za toleo la NOTE kuja na sifa hizi;
•    Kioo aina ya AMOLED inch 6.7fhd+
•    Mediatek Helio G96
•    30X Zoom Lens
•    120Hz
•    Camera tatu nyuma na Megapixel 64 camera kuu.
 
Kulingana na ukurasa wa @infinixmobiletz Infinix kwa kushirikiana na Tigo Tanzania kuzindua Infinix NOTE 11 na NOTE 11 pro Novemba 11 na watakuwa live kupitia kurasa zao za Instagram.

Bei ya simu hizi mbili bado kufahamika lakini inasadikia huenda bei ya Infinix NOTE 11 ikawa Tsh.470,000 na Infinix NOTE 11 pro Tsh.600,000 za Kitanzania. Kaa tayari kupokea mzigo mpya kutoka Infinix lakini pia unaweza tembelea https://www.infinixmobility.com/