MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wameingia mkataba wa miaka miwili na Kocha Pablo Franco Martín  raia wa Hispania kukinoa kikosi hicho kuanzia  Novemba 6, 2021.

Pablo anachukua nafasi ya Didier Gomes Da Rosa raia wa Ufaransa ambaye mkataba wake  ulisitishwa wiki mbili zilizopita baada ya makubaliano ya pande mbili.

Kabla ya kujiunga na Simba alikuwa anafundisha timu ya Al Qadsia SC ya Quwait kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.
 

Pablo mwenye umri wa miaka 41, mzaliwa wa Madrid,  alikuwa kocha Msadizi wa Real Madrid mwaka 2018 chini ya Kocha Julen Lopetegui na baadae Santiago Solari.

Mwaka 2015 alikuwa kocha wa Getafe inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania