Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO limezionya nchi kutoweka marufuku ya jumla ya kusafiri kutokana na kirusi kipya cha Omicron. 

Wanasayansi wanajaribu kubaini ni kiasi gani cha kinga ambacho chanjo za sasa zinaweza kutoa

Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO limezionya nchi kutoweka marufuku ya jumla ya kusafiri kutokana na kirusi kipya cha Omicron. 

Serikali mbalimbali na wanasayansi wanajaribu kubaini ni kiasi gani cha kinga ambacho chanjo za sasa zinaweza kutoa dhidi ya kirusi hicho. 

WHO imezitaka nchi kutumia mbinu ya ushahidi na athari zilizopo wakati wa kutangaza hatua zozote za kusafiri, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kuwachunguza au kuwaweka karantini abiria wa kimataifa. 

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema anafahamu kuna wasiwasi kuhusu Omicron, lakini marufuku ya jumla ya kusafiri haitokizuia kirusi hicho kusambaa. 

Kampuni ya BioNTech imeelezea matumaini kuwa chanjo inayotengeneza kwa ushirikiano na Pfizer inaweza ikatoa kinga imara dhidi ya Omicron. 

Visa vya kirusi hicho kipya vimesambaa, huku kisa cha kwanza kikiripotiwa Amerika Kusini nchini Brazil.